Version Conflict: Version Conflict: PROF.KABUDI: WATANGAZAJI MSIWE MOJA YA WATU WA KUFUBAZA NA KUDUMAZA KISWAHILI KWA KUTUMIA MANENO FASAHA NA SANIFU KATIKA LUGHA.

Na Debora Lemmubi,DmNewsonline

                   DODOMA 

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Paramagamba Kabudi amesema mbali na  utangazaji kuendana  na sauti inayovutia lakini ni vizuri kuwepo kwa matamshi fasaha sambamba na matumizi fasaha na sanifu ya lugha inayotumiwa katika Utangazaji.

Prof. Kabudi ameto kauli hii  mapema Leo Februari 13,2025 Jijini Dodoma katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa vyombo vya Utangazaji  Nchini ulioenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani.

Wàziri prof Kabudi amesema hivi karibuni  kumekuwa na changamoto ya kufubazwa na kudumazwa kwa kiswahili kwa kuyapa maana maneno yasiyostahili. Mfano uyu badala ya huyu au asira badala ya hasira.

Amesema Kuna haja ya  vyombo vya habari kuepuka kufubaza lugha ya kiswahili na kuhakikisha wanakuwa upande wa kusahihisha makosa hayo katika jamii. 

"Utangazaji huendana na sauti inayovutia na yenye kutamka matamshi kwa ufasaha na vile vile uwepo wa.matumizi fasaha ya lugha unayotumia kutangaza,ikiwa ni kiswahili basi kiwe kiswahili fasaha na sanifu ,ikiwa ni kingereza kiwe kingereza kiwe  sahihi ambapo tunajua kingereza sahihi ni kile kinachotoka Uingereza".amesema Prof Kabudi

Kumekuwa na changamoto katika kiswahili ya kufubaza na kudumaza kiswahili kwa kuyapa maana maneno yasiyo stahili maana hiyo".amesisitiza 

Pia  Waziri Kabudi  ametumia wasaa huo kutoa wito kwa Vituo vya utangazaji kutoa taarifa za mara kwa mara kwa wananchi na wakulima kuhusu utabiri wa hali ya hewa na athari za tabia ya Nchi,kwani Tanzania kupitia Mamlaka ya hali ya hewa ni miongoni mwa vyombo vya kisasa katika kutabiri mwenendo wa hali ya hewa nchini na Duniani.

 Naye Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt Jabir Bakari amesema kuwa jukwaa hili ni utaratibu ambao umewekwa na TCRA wa kukutana na vyombo vya Habari walau mara moja kwa mwaka ili kutafakari,kubadilishana mawazo na kupeana taarifa muhimu zinazoihusu Sekta ya Utangazaji. 

Kwaupande wake Gerson Msigwa ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kuandaa Jukwaa hilo na kutengeneza afua mbalimbali ambazo wanaamini  zitawasaidia watangazaji wanaokuja na kuweka mazingira mazuri ya kuwasaidia kufanya kazi zao kwa weledi.

"Kwani sasa ni tofauti na zamani ambapo mtu alikuwa anaweza kuwa mtangazaji pasipo kusoma ila kwa sasa hata atakuwa na uwezo au kipaji ni lazima pia apitie shuleni."amesema 

Awali akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo  amewakaribisha wageni wote waliohudhuria Mkutano huo wakiwemo wadau na wana tasnia ya Habari kutembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma kujionea miradi mikubwa na ya Kimkakati.

Amesema Moja ya maeneo ambayo wanaweza kutembelea ni Mahakama, uwanja wa Ndege inayotekelezwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Mkutano huu umewakutanisha Wamiliki, wadau na wana taaluma wa Masula ya Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Utangazaji ikiwemo Televisheni, Redio na Vyombo vya  habari vya Mitandaoni.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025