Version Conflict: MENEJA TIRA KANDA YA MASHARIKI AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKATA BIMA.AIPONGEZA SERIKALI

Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

           DAR ES SALAAM 

 MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ni taasisi ya Serikali ambayo  ilianzishwa kwa Sheria ya Bima Na.10 ya mwaka 2009 ikiwa chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Mamlaka ina majukumu ya kumlinda  mteja wa bima pia kuhakikisha kwamba wateja wa bima wanapata fidia stahiki na kwa wakati huku ikishughulikia malalamiko dhidi ya watoa huduma za bima pia inatoa miongozo mbalimbali kuhusu masuala ya bima pamoja na kutoa elimu ya bima kwa jamii.

TIRA pia inajukumu la kusajili makampuni ya bima yawe na leseni na kwa sasa yapo makampuni 40  na kuhakikisha yanatoa huduma bora kwa wananchi pamoja kuyatembelea makampuni hayo ili yaweze kulipa madai ya fidia kama inavyostahili na ukaguzi huo unafanyika mara kwa mara na kwa nyakati tofauti.

Akizungumza na Mwandishi wa habari kutoka  DmNews Online ,Meneja wa TIRA Kanda ya Mashariki Zakaria E.Muyengi amesema TIRA ina kanda mbalimbali ambapo Kanda ya Mashariki ina mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro na Pwani.

Amesema sehemu kubwa ya biashara ya bima ziko katika Kanda ya Mashariki yenyewe inabeba takribani asilimia 80 ya biashara ya bima.

Ameeleza kuwa Mamlaka hiyo ina wajibu wa kusajili makampuni ya kutoa huduma ya bima,kuwasimamia na kuhakikisha wanalinda haki  za wakata  bima pamoja na kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayohusu bima.

Amesema Kuna ofisi tatu za Mamlaka nazo ni Dodoma ambayo ndio Makao Makuu (headquarter)na subheadquqrter  ni Mtendeni Dar es Salaam pamoja na Zanzibar. 

Mamlaka ina Kanda 10 mbalimbali ikiwemo Kanda ya Mashariki,Kanda ya Kati (Dodoma,Iringa) ,Kanda ya Ziwa(Mwanza),Kanda ya Nyanda za Juu Kusini(Mbeya),Kanda ya Tanganyika (Rukwa),Kanda ya Pemba , Kanda ya Unguja na Kanda ya Kusini(Lindi na Mtwara).

Kuna aina tatu za Kampuni nazo ni Bima Mtawanyo,Bima ya Kawaida na Bima ya kati ,makampuni ya bima yako 40,Bima Mtawanyo yapo manne na jukumu lake kubwa nikuhakikisha haya makampuni mengine yanakuwa kushare risk yanapokuwa na majanga kupeleka kwenye makampuni mengine ikiwa ni pamoja nakusaidia mitaji ya ndani kuendelea kulipa madai ya ndani .

Hata hivyo Meneja amesema ni muhimu kwa wananchi kuwa na bima kwani zinasaidia pale unapopata changamoto yoyote ile inayohusu bima kuweza kulipwa fidia .

Amefafanua  kwa kueleza kuwa unapopata tatizo lolote la ajali na linahusu masuala ya Bima lazima uwe na viambatanisho ambavyo vitapelekwa kwenye kampuni husika ya bima yako ili ulipaji wa madai yawe rahisi.

TIRA imekuwa ikiambata na kushirikiana na wadau kama vile LATRA na Jeshi la Polisi kutoa elimu ya bima kwa wananchi na kutambua umuhimu wa kuwa na bima pia kutoa athari za kutembea ma chombo cha moto kisichokuwa na Bima.

Ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha kwa kutoa Bima ya Afya kwa wote

Hata hivyo Mamlaka itajitahidi kutoa elimu kwa kuyafikia makundi kama ya wasafirishaji,wakulima, wachimbaji wa madini,utalii,wanafunzi na waandishi wa habari ili waone Umuhimu wa  kutambua  kutumia bima.

Akizungumzia mafanikio Meneja Muyengi amesema  wamefanikiwa kwa asilimia 80 kwa makampuni yote kuwa na leseni na zimesajili kwa mujibu wa Sheria na kanuni pia usimamizi unafanyika pamoja na kutoa elimu kwa mikoa yote.huku wakiongozwa na KAULI MBIU ya ''TIRA kwa soko Salama la Bima'' 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025