Posts

Showing posts from February, 2025

WAZIRI KABUDI KUZINDUA BODI YA ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI MACHI 3.

Image
Na Mwandishi Wetu, JAB, Dar es Salaam WAZIRI  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi, Wiki ijayo anatarajiwa kuzindua Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB). Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali,  Gerson Msigwa imeeleza kuwa uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika  Machi, 03,2025 katika Hotel ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam. Katika Uzinduzi huo Waziri Kabudi pia atamkabidhi zana za Kazi Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Tido Mhando, zinazojumuisha Sera ya Habari, Sheria ya Huduma za Habari na Kanuni zake. Miongoni mwa majukumu ya Bodi hiyo yanayotarajiwa kuanza kutekelezwa mapema mara baada ya kuzinduliwa ni pamoja na kutoa Ithibati na Vitambulisho (Press Card) kwa Waandishi wa Habari waliokidhi vigezo vilivyoainishwa kisheria na kusimamia maadili ya taaluma ya Uandishi wa Habari. Kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229, Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imepewa mamlaka...

SERIKALI YAVUNA SHILINGI BILIONI 183 MASOKO YA MADINI

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline    WAKATI masoko ya madini yakifikia 43, mchango wa masoko hayo umeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 8 mwaka 2018/ 2019 hadi Shilingi Bilioni 183 mwaka wa fedha uliomalizika wa 2023/2024. Akizungumza katika mafunzo ya  matumizi ya mashine maalum ya kupima madini ya metali kwa njia ya MIONZI /X-RAY,  kwa maafisa masoko wa madini Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Venance Kasiki amesema mbali na masoko hayo pia kuna vituo vya ununuzi wa madini 109. Amesema, “Kwa kuzingatia asilimia kubwa ya mapato yetu katika masoko yanatokana na madini ya dhahabu, na ili tupate maduhuli lazima tutumie  mashine za XRF kupima asilimia (purity) ya madini yanayouzwa. Majibu yanayotokana na XRF yanatumika  kukokotoa mrabaha  na ada ya ukaguzi,”. Kwa upande wa Meneja wa Biashara ya Madini Sundi Malomo akizungumza amesema kuwa tangu Serikali kupitia Tume ya Madini  kuanzisha masoko ya madini Mei, 2019 kama mkakati wa kuimarisha bias...

HAFLA YA UZINDUZI USAMBAZAJI MITUNGI YA GESI

Image
Na Mwandishi Wetu, DmNewsOnline                      TANGA MATUKIO  mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa usambazaji mitungi ya gesi ya kupikia na majiko banifu kwa bei ya ruzuku inayofanyika leo Februari 27, 2025 mkoani Tanga.  Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.   Rais Samia leo hii amezindua ugawaji wa mitungi ya gesi (LPG) kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia

RAIS SAMIA AITAKA REA KUUPA KIPAUMBELE MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Image
Azindua mradi wa usambazaji nishati safi ya kupikia Sekta binafsi kupewa kipaumbele matumizi ya nishati safi kwa bei nafuu Apongeza ubunifu wa teknolojia za nishati safi ya kupikia Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                        TANGA  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuubeba mkakati wa nishati safi ya kupikia ili watanzania asilimia 80 watumie nishati safi na salama ifikapo 2034. Hayo yamebainishwa na Rais Dkt.Samia wakati wa uzinduzi wa usambazaji mitungi ya gesi ya kupikia na majiko banifu kwa bei ya ruzuku iliyofanyika leo Februari 27, 2025 wilaya ya Muheza mkoani Tanga.  "Niiombe wizara iendelee kusimamia vizuri, lakini niiombe REA iendelee na mkakati huu na sisi kwa ujumla kama Serikali tutaendelea kutunga Sera na Sheria zitakazotufanya tuende haraka na mkakati huu, " Amesema Rais Samia.   Vilevile ameongeza kuwa, Serikali itae...

WANANCHI WA KATA YA MISUGUSUGU NA VISIGA WAPATA ELIMU YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA

Image
Na Victor Masngu,DmNewsOnline,                    KIBAHA   BAADHI ya wananchi katika mitaa mbali mbali iliyopo katika  Kata za Visiga  na misugusugu katika Halmashauri ya Kibaha mji Mkoa wa Pwani wamepatiwa elimu bure juu ya msaada ya kisheria kuhusiana na masuala mbali mbali ikiwemo jinsi ya kutatua migogoro ya ardhi  pamoja na mambo  mengine ya mirathi pamoja na jinsi ya kuweza kupata haki zao za msingi. Akizungumza na baadhi ya wananchi  wa kata hizo  wakili George Banoba kutoka Wizara ya Katiba na sheria wakati wa Mwendelezo wa kampeni ya msaaada wa kisheria ya  Mama Samia amesema kwamba lengo kubwa ni kuwaelimisha wananchi juu ya kuweza kupata haki zao za msingi hasa katika suala zima la maeneo ya ardhi. Amesema kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto nyingi za wananchi kukosa msaada wa kisheria katika mambo mbali mbali ndio maana Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kuanzis...

TIC YASAJILI MIRADI 2020 JANUARI 2021 HADI JANUARI 2025 IKILINGANISHWA NA MIRADI 1,057 KWA MWAKA 2017 -2020.

Image
Na Deborah Lemmubi,DmNewsonline                     DODOMA MKURUGENZI  Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Gilead Teri ameeleza kuwa Taasisi hiyo imesajili miradi 2,020 ikiwa ni ongezeko la asilimia 91,katika kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2025 ikilinganishwa na miradi 1,057 iliyosajiliwa kwa mwaka 2017 hadi 2020 ambayo thamani ya miradi hii inakadiliwa kuwa Dola za Kimarekani Bilioni 23.67 ikiongezeka kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za kimarekani Bilioni 8.2 katika kipindi cha 2017-2020.  Teri ameyasema hayo leo februari 27,2025  jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo  akielezea mambo 10 muhimu na ya msingi yaliyotokea katika kipindi cha Uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.  Amesema  kumekuwa na ongezeko la asilimia 284.5 kutoka ajira 136,232 zilizozalishwa kipindi cha miaka minne ya kuanzia mwaka 2017 mpaka 2...

WANAFUNZI 2423 KATA YA TUMBI WAPIGWA MSASA JUU YA MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA

Image
Na Victor Masangu,DmNewsOnline                         KIBAHA  WANAFUNZI  zaidi ya elfu 2423 wa shule za msingi na sekondari zilizopo  Kata ya Tumbi katika Halmashauri ya Kibaha mji mkoani Pwani wamenufainika na kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Simia. Akizungumza na baadhi ya wanafunzi  kuhusiana na kampeni hiyo Wakili George Banoba kutoka Wizara ya Katiba na sheria amesema kwamba wamefanikiwa kupita katika shule mbali mbali zikiwemo shule za msingi tatu pamoja na shule ya sekondari Mwanalugali kwa lengo la kuweza kutoa elimu  ya  masuala mbali  mbali yanayohusiana na sheria. Banoba amebainisha kwamba katika kampeni hiyo wameweza kuambatana na wadau mbali mbali wa sheria akiwemo pamoja na Afisa ustawi wa jamii  pamoja na mkuu wa Dawati lajinsia Wilaya ya Kibaha kwa lengo la kuweza kupata  elimu kwa wanafunzi na kuwaajengea uwezo juu ya kutambua haki zao  za msingi ikiwemo m...

MATUMLA AMEWATA WATANZANIA KUJITOEZA KWA WINGI KWENYE PAMBANO LA FEBRUARI 28,MWAKA HUU.

Image
Na Mwandishi wetu ,DmNewsOnline                DAR ES SALAAM  BONDIA Amiri Matumla amewaomba watanzania kujitokezq kwa wingi kushuhudia pambano litakalofanya Februari 28,2025  dhidi ya mpimzani wa  kutoka Namibia ,Paul Amavila katika Ukumbi wa Magomeni Sokoni Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa Habari Februari 25, 2025 Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion, 'Knock Out ya Mama' Ally Zayumba na kufafanua kwamba bondia huyo katika pambano hilo atazichapa  na mpinzani wake kwa mizunguko nane. Zayumba amesema kwamba hili ni pambano lake la kwanza tangu ajiunge kwenye mapambano ya ngumi za kulipwa na ameahidi kufanya vizuri kwa lengo la kuanza kuweka rekodi nzuri katika karia yake kupitia masumbwi. Aidha, amesema katika  pambano hilo kutakuwa na mapambano mengine 11 ya utangulizi yakiongozwa na mkongwe Dullah Mbabe. Ameeleza kuwa huu ni msimu  tatu kwa mapambano ya aina hiyo kufanyika chini ya Mafia Boxing Prom...

WATU ZAIDI YA MIL.17 WANAPOTEZA MAISHA KWA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA IKIWEMO UGONJWA WA MOYO.-DKT KISENGE

Image
Na Deborah Lemmubi,DmNewsonline                    DODOMA  MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge ametoa ushauri kwa Tanzania kuhakikisha wanakula vyakula bora hasa vile vyenye protini, wanga na matunda kwa kiasi kikubwa. Pia matumizi ya mafuta ya nafaka kama vile alizeti na mahindi sambamba na kuacha uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kwa kiasi kidogo ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza kwani zaidi ya watu Milioni 17 hupoteza maisha kwa magonjwa yasiyoambukiza huku katika vifo hivyo vingi vikichangiwa na magonjwa ya moyo . Dkt Kisenge amesema hayo leo februari 26 ,2025 Jijini Dodoma  wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akielezea mafanikio ya taasisi hiyo ya JKCI kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.  Ameongeza kuwa kitu ambacho ni rahisi na kisicho na gharama ni ufanyaji wa mazoezi ambapo ameshauri kila mwananchi ambaye hana ch...