ORYX GES YAZIDI KUCHANJA MBUGA YAGAWA MITUNGI NA MAJIKO YAKE 1000 JIJINI MBEYA .
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgq1zY0YUx-mlSTjtyLJH5NYhXUEh490jrwPeAyiXN94cgkJi5Sz7utVdXz7uYzuN0ja6JV7YqMxwi7ntnH9jXiObZzLW2SAJy_Wf0P-CaCAqQ13WvFGqquPC3eVKktJq1HiYobZywGK0w/s1600/IMG_ORG_1725135836111.jpeg)
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline MBEYA SERIKALI imesema kuwa imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia nchini na lengo ifikapo 2034 asiliami 80 ya wananchi wawe wanatumia Nishati mbadala ya kupikia. Kauli hiyo imetolewa jijini mbeya Leo Agosti 31 ,2024 na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga wakati akikabidhi mitungi na majiko yake 1000 ambayo imetolewa na Kampuni ya Oryx Ges Kwa washiriki wa mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx jijini humo Kwa lengo la kuwawezesha kurahisisha shughuli za mapishi. Pia Naibu Waziri Kapinga amesema Serikali imewataka wadau wa gesi kuangalia uwezakano wa kuwa na gesi ambayo Mwananchi atanunua kidogo kidogo kila siku ilimkuwezesha wananchi wengi kutumia Nishati hiyo mbadala . Mashindano hayo ya kupika kwa gesi yaliyofanyika kuanzia Agosti 27 na kuhitimishwa leo Agosti 31,2024 yameandaliwa na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt.Tulia Akson kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ...