MNEC SALIM SAS KUIMARISHA CCM IRINGA



Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
IRINGA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM (MNEC) Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas anatarajiwa kufanya ziara  maalum katika mkoa huo ambayo inalenga kuimarisha Chama na kukutana na Halmashauri Kuu za CCM Wilaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Iringa imebainisha kuwa ziara hiyo inatarajia kuanzia Mufindi siku ya Jumamosi tarehe 3, Agosti mwaka huu.

"Agosti 3, 2024, Mufindi, Agosti 4  Kilolo, Agosti 7, Iringa Vijijini na mwisho atahitimisha Agosti 9, Iringa mjini," ilisema taarifa.

 MNEC ASAS ameendelea kukiimarisha chama katika Mkoa wa Iringa huku akiwa nguzo kwenye kushiriki miradi ya kimaendeleo kimkoa, Nyanda za Juu Kusini pamoja na Taifa kwa ujumla.

Pia ASAS anasifika kwa utendajikazi, upole, ustamilivu, subra, busara, huruma na mapenzi yake kwa chama na Taifa lake vimeendelea kumjengea taswira njema ya kwa wananchi wote.

Aidha, amekuwa mstari wa mbele kwa kujitolea katika sekta za afya, elimu, miundombinu, mitaji ya wafanyabiashara wadogo (Machinga), vijana na kinamama, lishe, mashuleni, michezo na mengine mengi.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025