Posts

Showing posts from February, 2024

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AFARIKI DUNIA LEO

Image
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza Kifo Cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi. Mzee Mwinyi amefariki hii Leo tarehe 29.02.2022 ambapo Siku Saba zimetangazwa kuwa siku za maombolezo.

RAIS SAMIA APELEKA BIL 23.6 KWA AJILI YA MAENDELEO KALIUA

Image
Na Allan Kitwe,DmNewsOnline KALIUA HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora imepokea zaidi ya sh bil 23.6 kutoka Serikali Kuu katika mwaka wa fedha 2023/2024 ili kufanikisha utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi. Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Japhael Lufungija alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji shughuli za maendeleo kwenye kikao cha baraza la madiwani katika kipindi cha miezi 3 kuanzia Okt-Des 2023. Amesema kuwa fedha hizo zimesimamiwa na kutumika ipasavyo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kulipa mishahara ya watumishi wa idara mbalimbali. Amebainisha kuwa kiasi hicho ambacho ni sawa na asilimia 56.8 ya bajeti yote ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ya sh bil 41.6, kimewezesha Wataalamu wa idara mbalimbali kutekeleza majukumu yao ipasavyo. ‘Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutuletea zaidi ya bil 23 kwa ajili ya utekelezaji shughuli za maendeleo ya wananchi ikiwemo kukamilisha baadh...

UCHORONGAJI VISIMA VYA JOTOARDHI KUANZA APRILI 2024

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  KENYA  NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa kazi ya uchorongaji wa visima vya Jotoardhi nchini Tanzania itaanza mwezi Aprili mwaka huu ili kuweza kuhakiki rasilimali ya Jotoardhi iliyopo kabla ya kuanza kwa shughuli za uzalishaji umeme kutokana na nishati hiyo. Dkt. Biteko amesema baada ya kutembelea vyanzo na mitambo ya kuzalisha umeme wa Jotoardhi katika Mji wa Naivasha, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya. “Tumekuja kwenye mitambo ya kuzalisha umeme unaotokana na Jotoardhi inayomilikiwa na kampuni ya uzalishaji umeme ya Kenya (KenGen) na tumejionea jinsi walivyopiga hatua kwenye uendelezaji wa rasilimali hii kwani tayari wanazalisha umeme wa Jotoardhi wa kiasi cha megawati zaidi ya 799.” Amesema Dkt. Biteko Amesema Tanzania kwa upande wake, tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya kuendeleza vyanzo vya Jotoardhi na kwamba kampuni ya KenGen mwezi Aprili mwaka huu itakuwa mkoani Mbeya kwa ajili ya kuanza uchor...

MIZIMU YA KATABI HIFADHI YA TAIFA KATAVI YAWAKIVUTIO KIKUBWA CHA UTALII.

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  KATAVI IMEBAINISHWA  kuwa Hifadhi ya Taifa Katavi ni moja ya Hifadhi ambayo inavivutio vingi vya utalii ikiwepo kivutio kikubwa cha ziwa katavi ambalo limebarikiwa kuwa na viboko wengi sana ukilinganisha na maeneo mengine . Hayo yamebainishwa februari 28 ,2024 na Afisa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa Katavi Beatrice Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo mkoani humo kwalengo la kuuzungumzia utalii wa hifadhi hiyo ya katavi. Amesema kuwa Hifadhi ya taifa Katavi inasifika sana Kwa uwepo wa viboko wengi hasa kupitia ziwa katavi lakini  licha ya kusifika na kuwa na viboko wengi kupitia ziwa katavi lakini Kuna vivutio vingine Kama wanyama mbalimbali . Beatrice ametaja  vivutio vingine ni uwepo wa Simba ambao wanatembea Kwa makundi, Twiga, Swara ,Tembo, Chuwi, Pundamilia, lakini Kuna aina mbalimbali za ndege. Ameongeza kuwa Katika Hifadhi ya taifa katavi pia ina Uvuvi wa samaki Kwaajili tu ya .... na hakuna ruhusa ya kum...

EMIRATES FULL ACQUIRES BUSTANICA WORLD LARGEST INDOOR VERTICAL FARM

Image
DmNewsOnline. Emirates Flight Catering, one of the world’s largest catering operations, has fully acquired Emirates Bustanica, formerly called Emirates Crop One, and its consumer brand Bustanica, the world's largest indoor vertical farm. This strategic move establishes Emirates Bustanica as a fully UAE-owned company, helping sustain the country's vision of enhancing food and water security and its agricultural capabilities.  The acquisition empowers Emirates Bustanica to leverage its local expertise and the latest tech know-how to meet the growing demands of the market.Emirates Flight Catering (EKFC) is one of the world’s largest catering operations.Offering airline, events and VIP catering as well as ancillary services including laundry, food production and airport lounge food and beverage.  A trusted partner EKFC, serves over 100 airlines, hospitality groups and United Arab Emirates government entities.  Each day, the company’s 11,000 dedicated employees prepare an aver...

EMIRATES YANUNUA SHAMBA KUBWA ZAIDI LA UZALISHAJI MAZAO YA CHAKULA

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline.  Emirates Flight Catering, mojawapo ya kampuni kubwa zaidi za upishi duniani, imenunua Emirates Bustanica, ambayo zamani iliitwa Emirates Crop One, na chapa yake ya watumiaji wa Bustanica, shamba kubwa zaidi la wima la ndani.  Hatua hii ya kimkakati inaanzisha Emirates Bustanica kama kampuni inayomilikiwa kikamilifu na UAE, na kusaidia kuendeleza dira ya nchi ya kuimarisha usalama wa chakula na maji na uwezo wake wa kilimo. Ununuzi huo unaipa Emirates Bustanica uwezo wa kutumia talalamu wake wenyeji na ujuzi wa kisasa wa teknolojia ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya soko. Emirates Flight Catering (EKFC) ni moja wapo ya makampuni kubwa zaidi za upishi duniani. Kutoa mashirika ya ndege, matukio na upishi wa VIP pamoja na huduma za ziada ikiwa ni pamoja kufua nguo, kupika cha sehemu za mapumziko ya uwanja wa ndege na kutengeneza vinywaji. Kama kampuni ya ndege anayeaminika EKFC, huhudumia zaidi ya makampuni za 100, vikundi vya ukarimu na mashir...

MADIWANI KALIUA WASIKITISHWA KUCHELEWA MIRADI YA MAJI

Image
Na Allan Kitwe,DmNewsOnline  KALIUA  MADIWANI wa halmashauri ya Wilaya Kaliua Mkoani Tabora wamemtaka Meneja wa Wakala wa Maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijini Wilayani humo kuhakikisha miradi yote iliyokwama inatafutiwa ufumbuzi ili ikamilike. Wakizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo jana wameeleza kusikitishwa na baadhi ya miradi ikiwemo ya uchimbaji mabwawa na visima katika vijiji mbalimbali kukwama kwa mda mrefu hali inayoibua maswali. Akizungumza katika Kikao hicho diwani wa Kata ya Kazaroho, Haruna Kasele amesema kuwa Meneja amekuwa akitoa maelezo mazuri ya kutekelezwa miradi hiyo lakini cha kusikitisha hakuna kinachoendelea na miradi haikamiliki. ‘Tunataka kusikia mikakati ya kumaliza kero ya maji katika maeneo yote yanayolalamikiwa ikiwemo kata ya Makingi, Ichemba na kwingineko, tumechoka hadithi za kwenye makaratasi, uchaguzi umekaribia tutasema nini’, ameema. Diwani wa Kata ya Ichemba katika tarafa ya Ulyankulu, Juma Hamduni amesema ku...

MAAFISA HABARI WATAKIWA KUTANGAZA MIRADI YA SERIKALI

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline         MAAFISA Habari Serikalini wameagizwa  kutangaza miradi na shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili wananchi wajue ikiwemo  kujibu hoja za uongo zinazotolewa na watu dhidi ya serikali . Akifungua Mkutano wa siku tatu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Dkt.Damas Ndumbaro kwaniaba ya Naibu Waziri Mkuu,Doto Biteko. Amesema maofisa hao wanawajibu mkubwa wakutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili watu waone ukubwa wa kazi zinazofanywa na serikali katika nchi hii "Baadhi ya watu hawaoni ukubwa wa katarasi nyeupe ulivyo sasa ni wajibu wenu kueleza kazi zinazofanywa na serikali ikiwemo kujibu hoja za uongo dhidi ya serikali lazima mjue kujibu fitna na zengwe"Amesema  Amesema hata serikali inapigwa fitna sasa ni kazi yenu kujibu fitna na zengwe kwani hivi sasa zama za teknolojia ya habari imekua na ni nzuri ila inachangamoto zake kupitia mitanda...

VIONGOZI WA DINI WAOMBWA KUAMASISHA JAMII KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  VIONGOZI wa dini nchini wameombwa kushiriki kikamilifu katika kuimasisha jamii kuchana na uharibu wa mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa katika kuandaa chakula. Ombi hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya Oryx 1000 pamoja na majiko yake kwa viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali mkoani Kilimanjaro yaliyokwenda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya matumizi ya nishati safi ili kuepuka madhara kwa jamii. Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema viongozi wa dini wanamchango mkubwa katika kusaidia jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuachana kutumia kuni na mkaa. Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Benoite Araman ametumia nafasi hiyo kueleza  kwa muda mrefu sasa wamekuwa wanajivu...

UJUMBE WA TANZANIA WAJIFUNZA UTENGENEZAJI VIFAA VYA UONGEZAJI THAMANI VITO

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline BANGKOK NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo mwishoni mwa wiki aliongoza Ujumbe wa Tanzania nchini Thailand kutembelea Kiwanda Earth Supply Co. Ltd  kinachotengeneza Mashine zinazotumika katika shughuli za kukata, kutoboa na kunga’risha madini ya Vito. Ziara katika kiwanda hicho ililenga kujifunza kuhusu teknolojia mbalimbali za kisasa zinazotumika katika shughuli hizo ikikumbukwa kwamba, Thailand ni miongoni mwa nchi zilizoendelea katika shughuli za uongezaji thamani madini ya vito zikihusisha utengenezaji wa bidhaa za mapambo ya vito na usonara ya thamani kubwa. Katika ziara hiyo ilielezwa kwamba, nchi walaji wa mashine zinazotengenezwa na kiwanda hicho ni pamoja na Colombia, Uswis, Madagascar na Thailand yenyewe ambapo shughuli hizo zimeshamiri kwa kiasi kikubwa. Pia , ziara hiyo kiwandani hapo ni mwendelezo  wa dhamira na jitihada zinazofanywa na Serikali kusimamia shughuli za uongezaji thamani madini ya vito na usonara ikiwemo ku...