BUJURA YAMSINDIKIZA MALONGO KWA SHANGWE KUREJESHA FOMU YA UDIWANI

Na Mwandishi wetu, DmNewsonline GEITA Mgombea udiwani wa Kata ya Bujura kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Malongo Mahamed Salum, leo Agosti 27, 2027, amerejesha fomu ya kugombea udiwani huku akisindikizwa na wananchi wa vijiji vyote vya Ngura kwa bashasha, vifijo, nderemo na shangwe mpaka ofisi za kata. Baada ya kurejesha fomu, Malongo ameahidi kushirikiana kwa karibu na wananchi katika shughuli za maendeleo pamoja na kushirikiana nao katika shida na raha za kila siku. Aidha, aliahidi ushirikiano na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo ili kupunguza changamoto zinazowakabili wananchi wa Kata ya Bujura. Katika uchaguzi wa kura za maoni, Malongo aliibuka kidedea baada ya kupata kura 434 kati ya kura 513 zilizopigwa, akiwashinda Bundala Charles aliyepata kura 35 na diwani mstaafu Amina Kanijo aliyepata kura 41.