Posts

Showing posts from March, 2025

RAIS DKT SAMIA AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUSALI KATIKA IBADA YA IDD MSIKITI WA MOHAMED VI KINONDONI.

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                     DAR ES SALAAM  RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  akijumika na waisalamu wengine  kusali swala ya Eid katika kukamilisha ibada ya Mfungo wa Ramadhan katika Msikiti wa Mohamed VI uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Kinondoni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuswali Swala ya Eid El Fitr tarehe 31 Machi, 2025.

EWURA KINARA UHUSIANO MWEMA NA VYOMBO VYA HABARI.

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsonline KWA mara ya pili mfululizo, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeshinda tena tuzo ya Uhusiano Mwema na Vyombo vya habari nchini, kwa mwaka 2024. Ushindi huo umedhihirisha namna taasisi hiyo inavyothamini ushirikano na uhuru wa vyombo vya habari katika kuuhabarisha umma kuhusu shughuli za udhibiti wa huduma za nishati na maji.  Tuzo hiyo iliyotolewa jana(29.3.2024) na Chama cha Maofisa Uhusiano Tanzania (PRST), baada ya mchuano mkali uliohusisha taasisi nyingi. Tuzo hiyo imeipa EWURA heshima na ari ya kuendelea kudumisha uhusiano wake thabiti na vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari nchini. Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo alisema ushindi huo kwa mara ya pili mfululizo ni kielelezo cha utawala bora, uwazi, uwajibikaji, na miongozo inayotolewa na Bodi na Menejimenti ya EWURA, chini ya Mwemyekiti wake Prof. Mark Mwandosya na Mkurugenzi wake Mkuu, Dkt. James Mwainyekule.  Vigezo vilivyotumika kuipa...

POLISI DAR YATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUTOWAACHA WATOTO KWENDA KATIKA KUMBI BILA UANGALIZI

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline          DAR ES SALAAM  JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limetoa  wito kwa wazazi na walezi kutowaacha watoto kwenda katika kumbi na maeneo mbalimbali bila kuwa na uangalizi kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea watoto kupotea,kupata ajali au kufanyiwa  vitendo vinavyoweza kuhatarisha afya na maisha yao. Hayo yamebainishwa Machi 30,2025,Jijini  Dar es Salaam na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ,SACP Muliro Jumanne Muliro wakati akizungumza na wanahabari amesema kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vingine vya dola linaendelea kuimarisha usalama na linapenda kuwafahamisha wakazi wa Dar es Salaam kuwa Jiji lipo shwari. Aidha,amesema Polisi Dar es Salaam inatambua kuwa tarehe 31,Machi 2025 au Aprili 1,2025 kutakuwa na sikukuu ya Eld-el-fitri kutegemea kuandama kwa mwezi.Kutokana na umuhimu wa sikukuu hiyo ,suala la usalama limewekewa uzito mkubwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji...

WATU WANNE SAME WAPANDISHWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MOSHI KWA UHUJUMU UCHUMI.

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                    SAME  WAKAZI wanne wa Wilaya ya Same wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi  Machi 28, 2025, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi,kwakudaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa jumla ya kilogramu 518.57. Watuhumiwa hao, Nimkaza Mbwambo, Prosper Lema, Nterindwa Mgalle, na Stephanie Mrutu, walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ally Mkama. Wakili wa Serikali, Julieth Komba, aliwasomea mashitaka kwa nyakati tofauti ambapo alidai kuwa, Machi 21, 2025, watuhumiwa hao walitenda makosa hayo katika kijiji cha Rikweni, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro. Katika mashitaka, ilidaiwa kuwa mshitakiwa Nimkaza Mbwambo alikamatwa akisafirisha kilogramu 138.58 za dawa za kulevya aina ya mirungi, huku Prosper Lema naye akikamatwa akiwa na kilogramu 113.29. Pia, Nterindwa Mgalle alikamatwa akiwa na kilogramu 160.25 za mirungi, wakati Stephanie Mrutu aliku...

WAZIRI MAVUNDE ASISITIZA MIRADI MIKUBWA YA MADINI ILIYOPEWA LESENI KUANZA KAZI HARAKA

Image
Na Mwandishi wetu, DmNewsOnline Dodoma Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameagiza Miradi Mikubwa na ya Kati ya madini ambayo tayari imekwishapewa leseni kuanza utekelezaji wake mara moja ili kuchochea ukuaji wa sekta na kuleta manufaa kwa taifa kwa ujumla na kutimiza azma ya Serikali kutoa leseni hizo. Amesema hayo, leo Machi 28, 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika Mkutano maalum na Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) kwa lengo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini ili kuboresha uendelezaji na usimamizi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa manufaa ya sekta na taifa kwa ujumla, ikiwa ni sehemu ya ratiba yake ya kukutana na makundi yote yayojihusisha na mnyororo mzima wa Sekta ya Madini nchini. Waziri Mavunde amesema Serikali inataka kuhakikisha kuwa Miradi yote ya Uchimbaji Madini iliyopangwa kuanza inaanza mara moja bila kucheleweshwa, na kuwa Serikali kwa upande wake imejitahidi kurahisisha taratibu kwa wawekezaji na sasa ni wakati wa Sekta b...

ABSA DAR CITY MARATHON SASA KUFANYIKA 04/05/2025 | WANANCHI WAHIMIZWA KUSHIRIKI MBIO HIZO

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline Dar Es Salaam The Runners Tanzania wamezindua rasmi Absa Dar City Marathon 2025, ikiwa ni msimu wa tano wa mbio hizo, zitakazofanyika Mei 4, 2025, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Lengo kuu la mbio hizi ni kusaidia mahitaji ya Hospitali ya Mnazi Mmoja. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Godfrey Mwangungulu, Makamu Mwenyekiti wa Runners Club, amesema wanatarajia washiriki wasiopungua 3,000 msimu huu na amewasihi watu kuendelea kujisajili kwa ada ya shilingi 40,000. “Tunakwenda kufanya msimu wa tano wa Dar City Marathon, mbio ambazo zimekuwa zikifanyika kwa mafanikio na kuendelea kukua mwaka hadi mwaka. Mwaka huu tunatarajia washiriki zaidi ya 3,000,” alisema Mwangungulu. Aliendelea kusisitiza kuwa mbio hizi si za mashindano tu, bali pia ni fursa ya kujenga mshikamano na kusherehekea pamoja. Kwa upande wake, Aron Luhanga, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Absa Bank, amesema benki hiyo kama mdhamini mkuu imejipanga vyem...

WAFUGAJI KIBAHA NA BAGAMOYO WAANZA KUPATA NEEMA YA MIFUGO YAO BAADA YA SERIKALI KUWAPATIA CHANJO LAKI 178

Image
Na Victor Masangu,Dmnews,Online                 KIBAHA  SERIKALI  ya awamu ya sita kupitia wizara yake ya mifugo na uvuzi imeanza kutekeleza azma yake ya mpango wa kuwasaidia wafugaji  ambapo imetoa chanjo dozi 178,000 kwa halmashauri ya wilaya Kibaha na Bagamayo kwa ajili ya  mifugo  yao ikiwa ni moja ya chanjo zinazotolowe katika   kampeni ya kitaifa kwa ajili ya uchanjaji wa mifugo hiyo ambayo  lengo lake kubwa ni kuweza kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo hapa nchini. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi  wa Operesheni   kutoka  kiwanda cha chanjo za wanyama cha Hester Biosciences  Afrika Limited ambacho ndio kinatengeneza chanjo hizo Ms. Chistine Sokoine wakati wa halfa ya kukabidhi chanjo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha pamoja na Bagamoyo.  Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba  wamefanikiwa kutoa chanjo hizo zipatazo dozi 178,000 ambazo ni za aina mbili ikiwem...

MAKAMU WA RAIS DKT.MPAMGO KUZINDUA MWENGE WA UHURU KITAIFA APRIL 2 PWANI

Image
Na Victor Masangu,DmNews,Online                      PWANI  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mbio za mwenge  kitaifa utakaofanyika katika viwanja vya shirika la Elimu Kibaha Mkoani Pwani, Aprli 02,2025. Hayo yamebaishwa na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kutembelea na  kukagua  maandalizi ya uzinduzi wa Mwenge wa uhuru ambapo ameridhishwa na maandalizi yalipofikia. Amesema uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2025 utakuwa Aprli 02 katika viwanja vya shirika la elimu kibaha na kwamba mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa jamuuri ya muungano wa Tanzania Dk Philip Isdor Mpango. Aidha amesema baada ya mbio hizo kuzinduliwa, mgeni huyo rasmi atawakabidhi viongozi sita wa mbio za mwenge walioandaliwa k...