SERIKALI YAKEMEA VITENDO VYA UTEKAJI NA UNYANYASAJI KWA WATOTO

Na Angelina Mganga,DmNewsOnline DAR ES SALAAM WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali haikubaliani na vitendo vyote vya utekaji na unyanyasaji wanavyofanyiwa baadhi ya watoto kwani vitendo hivyo viovu vinaenda kinyume na utamaduni wa Taifa lenye utu, ustaarabu, amani na utulivu. Hayo yamebainishwa leo Julai 28,2024 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Masauni wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu matukio ya vitendo vya ukatili na utekaji wa watoto amesema serikali imechukua hatua stahiki kwa wale wote waliobainika na itaendelea kuwachukulia hatua wale watakaobainika. “Hatua Kali zitachukiliwa Kwa wale wote watakaobainika kuhusika na matukio haya ya kihalifu na tunaungana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan na watanzania wote wakiwemo wazazi na walezi kukemia vikali matukio haya ya kihalifu kwa watoto “ amesema Waziri Mhandisi Masauni. Aidha, ametoa rai kwa wananchi kushirikiana na Serikali husus...